Umoja wa Mataifa: Israel inapaswa kusitisha harakati zake nchini Syria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i119990-umoja_wa_mataifa_israel_inapaswa_kusitisha_harakati_zake_nchini_syria
Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Syria ametaka kusitishwa harakati za utawala wa Israel nchini Syria.
(last modified 2024-12-11T00:57:33+00:00 )
Dec 11, 2024 00:57 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Israel inapaswa kusitisha harakati zake nchini Syria

Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Syria ametaka kusitishwa harakati za utawala wa Israel nchini Syria.

Geir O. Pedersen ameongeza kuwa Syria sasa iko katika njia panda na hatua za sasa za Israel katika nchi hiyo lazima zikomeshwe.

Akisisitiza udharura wa kufanyika maandalizi ya kukabidhi madaraka kwa kushirikisha taifa zima la Syria, Pedersen ameonya dhidi ya hatari ya kutokea machafuko zaidi nchini humo iwapo makundi yote ya Wasyria hayatashirikishwa katika serikali ijayo.

Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria hapo awali alisisitiza kwamba Wasyria wote wanapaswa kutoa kipaumbele kwa mazungumzo, umoja na kuheshimu sheria za kimataifa, na ametoa wito wa kuanza mchakato wa utawala wa mpito nchini Syria.

Baada tu ya kuanguka utawala wa Syria, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel lilianza kushambulia maeneo mbalimbali ya nchi hiiyo na hadi sasa limevamia na kukalia kwa mabavu baadhi ya mikoa ya nchi hiyo.