Wananchi wa Marekani hawana imani na serikali na vyombo vya habari
Matokeo ya uchunguzi wa maoni wa karibuni yanaonyesha kuwa kutokuwa na imani wananchi wa Marekani na serikali ya Joe Biden na kwa vyombo vya habari kulitayarisha mazingira ya ushindi wa "Donald Trump" na Warepublican katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na Taasisi ya Utafiti ya Schoen Cooperman kwa ushirikiano na uongozi wa Kitengo cha Usimamizi na Mawasiliano ya Kistratejia cha Chuo Kikuu cha George Washington yamefichua mwekeleo mpya wa sababu zilizopelekea Wademocrat kushindwa katika uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka huu.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni, kutokuwa na imani wananchi wa Marekani na serikali ya Biden na vyombo vya habari ni moja ya sababu kuu za ushindi wa Trump na chama cha Republican katika uchaguzi wa rais wa 2024.
Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yamesisitiza kuwa Wademocrat walifanya makosa na kwa utaratibu huo wapiga kura Marekani walifadhilisha kumpigia kura Donald Trump.
Matokeo haya ya uchunguzi wa maoni, asilimia 39 ya wananchi wa Marekani wamesema kuwa hawana imani na serikali, huku asilimia 41 kati yao wakiwa na imani ndogo kwa serikali katika suala la kutoa taarifa zilizo sahihi.
Kuhusu suala la uaminifu na habari sahihi wakati wa uchaguzi wa 2024, asilimia 69 au karibu saba kati ya kila watu 10 wa Marekani wanaamini kwamba taarifa za uongo zimefanya iwe vigumu kupata habari sahihi na za kweli.
Pia, asilimia 71 wametaja wasiwasi wao kuhusu maudhui ghushi (deepfake) kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2024.