Wabunge wa Marekani wamtaka Biden aache kuipatia silaha Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i120322-wabunge_wa_marekani_wamtaka_biden_aache_kuipatia_silaha_israel
Wabunge nchini Marekani wamemuandikia barua Rais Joe Biden wa nchi hiyo wakimtaka asitishe kuupatia silaha utawala haramu wa Israel.
(last modified 2024-12-18T23:39:39+00:00 )
Dec 18, 2024 23:39 UTC
  • Wabunge wa Marekani wamtaka Biden aache kuipatia silaha Israel

Wabunge nchini Marekani wamemuandikia barua Rais Joe Biden wa nchi hiyo wakimtaka asitishe kuupatia silaha utawala haramu wa Israel.

Katika barua yao wabunge 20 wa Marekani wameutaka utawala wa Rais Joe Biden kuacha kutuma "silaha za mashambulizi" kwa utawala wa Kizayuni ambao unazitumia kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.

Greg Kasar mmoja wa Wabunge hao kutoka chama cha Democrats katika Baraza la Wawakilishi la Marekani, ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba yeye na wabunge wengine 19 wa nchi hii wameitaka serikali ya Biden kusitisha hatua zake za kuipatia silaha Israel.

Mwakilishi huyu wa jimbo la Texas aliongeza kuwa, sheria ya Marekani iko wazi; Iwapo serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu haitaruhusu chakula na dawa za kutosha kuingia Gaza, Marekani haipaswi kupeleka silaha huko.

Sehemu moja ya barua hiyo ya wabunge 20 wa Marekani inasema kuwa, utawala wa Biden umeiomba Israel kuruhusu angalau malori 350 ya misaada kuingia Gaza kila siku, lakini Israel inaruhusu malori 42 tu kuingia Gaza kila siku kiwango ambacho ni kidogo sana ikilinganishwa na mahitaji ya wakazi wa Ukanda huo.

Hivi karibuni Bunge la Seneti la Marekani lilipinga maazimio ya kusimamisha uuzaji wa baadhi ya silaha kwa utawala wa Kizayuni ambayo yaliwasilishwa kutokana na wasiwasi wa ukiukwaji wa haki za binadamu na ongezeko la mauaji ya raia wa Palestina. Hatua hiyo kwa mara nyingine tena ilithibitisha uongo wa Marekani kwamba, ni mtetezi wa haki za binadamu.