Haki za binadamu; wenzo wa kisiasa wa madola ya Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i120392-haki_za_binadamu_wenzo_wa_kisiasa_wa_madola_ya_magharibi
Canada, kama ilivyokuwa katika miaka ya hivi karibuni, imewasilisha kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa rasimu ya azimio kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu nchini Iran na kupasishwa kwa mbinde katika kamati ya tatu ya Baraza Kuu.
(last modified 2024-12-20T23:22:33+00:00 )
Dec 20, 2024 23:22 UTC
  • Haki za binadamu; wenzo wa kisiasa wa madola ya Magharibi

Canada, kama ilivyokuwa katika miaka ya hivi karibuni, imewasilisha kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa rasimu ya azimio kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu nchini Iran na kupasishwa kwa mbinde katika kamati ya tatu ya Baraza Kuu.

Azimio hilo dhidi ya haki za binadamu la Iran liliidhinishwa kwa kura 77 za ndio huku idadi ya kura za hapana zikiwa 22 na nchi 66 hazikuweko katika zoezi la upigaji kura na kufanya idadi ya kura hizo kwa pamoja kuwa nyingi kuliko kura za ndio zilizopasisha azimio hilo.

Katika radiamali yake ya kupasishwa azimio hilo, Esmail Baqaei msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeonyesha kutoridhishwa kwao na kutumiwa vibaya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa: Hatua hizo zisizo na uhalali zinazochukuliwa na baadhi ya watendaji ambao wenyewe wana historia ndefu ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ukiwemo uungaji mkono wa kisilaha na kisiasa kwa uvamizi na mauaji ya kimbari huko Palestina, sio  kwamba, hazisaidii kuboresha hali ya haki za binadamu na kuheshimiwa hilo katika ngazi ya kimataifa, bali kimsingi zinahafifisha na kuudhhoofisha dhana na maana ya haki za binadamu na kushusha haadhi yake na hivyo kukifanya kuwa chombo na wenzo wa mashinikizo ya kisiasa dhidi ya mataifa mengine.

Eneo la makaburi ya umati ya watoto wa wenyeji asili wa Canada 

 

Katika miaka ya hivi karibuni, hakuna suala ambalo limetumiwa kisiasa na serikali za Magharibi kwa ajili ya kuendeleza malengo yao yasiyo ya kibinadamu kama kadhia ya haki za binadamu. Kila mwaka, kwa kuzingatia nia na utashi wa kisiasa, Canada huwasilisha azimio dhidi ya Iran kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ikidai ukiukaji wa haki za binadamu nchini Iran. Maazimio haya huchunguzwa kwanza katika kikao cha kamati ya tatu ya Baraza Kuu na hatimaye kupelekwa Baraza Kuu kwa ajili ya kupigiwa kura.

Azimio dhidi ya Iran lililowasilishwa na Kanada limepasishwa katika hali ambayo utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ukiungwa mkono kikamilifu na waandaaji wa azimio hilo dhidi ya Iran umeanzisha maonesho ya jinai dhidi ya binadamu. Kwa hakika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, hakuna jinai yoyote ya kivita huko Gaza ambayo haijafanywa na utawala huo ghasibu.

Katika kipindi hiki, Israel imetekeleza mauaji ya halaiki na mauaji ya kimbari na kikaumu  dhidi ya watu wanaodhulumiwa wa Gaza na inaendelea kuwaua bila kuchoka raia wakiwemo wanawake na watoto wasio na hatia. Zaidi ya watoto 17,000 wa Kipalestina wameuawa  hadi sasa huku takwinmu zikionyesha kuwa, kila dakika kumi mtoto mmoja wa Kipaalestina anauawa huko Gaza na Wazayuni.

Mamia ya watoto wachanga wanauawa muda mfupi baada ya kuzaliwa kutokana na mashambulizi ya mabomu katika maeneo ya makazi, hospitali, shule, mahema ya wakimbizi sambamba na uharibifu wa vituo vya huduma za afya.

Je, mauaji ya raia, wakiwemo wanawake na watoto wasio na hatia, uchomaji moto wa kutisha wa watoto mbele ya mama zao, ulipuaji wa shule, hospitali na mahema ya wakimbizi hautoshi kwa nchi zinazodai kuutetea haki za binadamu ili kuitisha mkutano maalum katika Baraza la Baraza la Haki za Binadamu?

Hivi haujafika wakati wa kuundwa kamati ya kutafuta ukweli na kuwasilisha kwa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu na hivyo kuupasishwa azimio la haki za binadamu dhidi ya mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita huko Gaza?

Moja ya shule za kulea watoto Canada ambamo ndani yake watoto wengi walikabiliwa na vitendo vya unyanyasaji, ubakaji na ulawiti

 

Canada ni mojawapo ya nchi zinazopigia upatu suala la haki duniani. Lakini cha ajabu, Canada imekuwa ikitoa himaya na uungaji mkono kwa utawala wa Kizayuni ambao unafanya mauaji ya kimbari dhidi ya watoto huko Gaza. Waidha yenyewe Canada ina ina historia mbaya ya kukiuka haki za binadamu. Rekodi ya haki za binadamu ya Canada imejaa orodha ndefu ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika nyanja mbalimbali. Kufichuliwa mauaji ya wakazi asilia wa Canada, hasa watoto, kumeibua kashfa kubwa dhidi ya nchi hiyo inayodai kuwa mtetezi wa haki za binadamu ulimwenguni.

Aidha kugunduliwa makaburi ya umati nchini Canada katika miaka ya karibuni limegeuka kuwa suala zito na muhimu linalojadiliwa na waliowengi ulimwenguni.

Ushahidi wa kihistoria na kugunduliwa makaburi ya umati katika mikoa tofauti ya Canada unathibitisha wazi kwamba kwa miongo kadhaa, siasa kuu za serikali na Kanisa Katoliki zilikuwa ni kupora ardhi na rasilimali za wenyeji, kutenganisha watoto na familia zao pamoja na kuharibu lugha, tamaduni, mila na ustaarabu wao. Siasa hizo zilitekelezwa kwa kuwatenganisha watoto wa wakazi asilia na familia zao na kisha kuwalazimisha kuishi kwenye shule za bweni ambapo walibadilishwa fikra na kulazimishwa kuiga tamaduni za wageni waliowakoloni.

Wengi wa watoto hao walikabiliwa na unyanyasaji, ubakaji, ulawiti na utapiamlo katika shule hizo, kiasi kwamba mamia miongoni mwao walikufa kwa magonjwa, utapiamlo na kupuuzwa hali zao za kiafya na kisha kuzikwa kwenye makaburi mahsusi au ya umati bila kutajwa majina wala anwani yoyote.

Canada, ikiwa ni nchi inayodai kuwa mtetezi wa haki za binadamu, kwa kuwasilisha azimio dhidi ya Iran katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, inakusudia kuwahadaa walimwengu, kupotosha fikra na maoni ya umma na kufunika nafasi yake ya ushirikiano na Wazayuni katika mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.