Kuongezeka uhalifu wa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i120862-kuongezeka_uhalifu_wa_vitendo_vya_chuki_dhidi_ya_uislamu_nchini_uingereza
Baraza la Kiislamu la Uingereza limetangaza kuwa vitendo vya uhalifu dhidi ya Uislamu vimeongezeka sana katika baadhi ya maeneo nchini humo.
(last modified 2025-01-01T00:11:36+00:00 )
Jan 01, 2025 00:11 UTC
  • Kuongezeka uhalifu wa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini Uingereza

Baraza la Kiislamu la Uingereza limetangaza kuwa vitendo vya uhalifu dhidi ya Uislamu vimeongezeka sana katika baadhi ya maeneo nchini humo.

Takwimu za karibuni za Wizara ya Mambo ya Ndani na ripoti za taasisi huru zinazofuatilia ubaguzi na chuki dhidi ya dini mbalimbali nchini Uingereza zinaonyesha kuwa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu vinaongezeka kwa kasi kubwa dhidi ya Waislamu wanaoishi nchini humo. 

Huku ikitegemea ripoti ya polisi ya mji wa Manchester kuhusu kuongezeka uhalifu wa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu, Baraza la Kiislamu la Uingereza limetangaza kuwa uhalifu unaohusiana na chuki dhidi ya Uislamu umeongezeka kutoka kesi 39  hadi kesi 85 kwa mwezi. 

Takwimu hizo zinaonyesha kuongezeka upuuzaji ulioratibiwa wa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu kama aina ya ubaguzi wa rangi; hali ambayo inaonyesha kuwa ipo haja kwa serikali ya Uingereza kuchukua hatua za haraka na kali kukabiliana na hujuma hizo.   

Chuki dhidi ya Uislamu yakiri nchini Uingereza 

Baraza la Kiislamu la Uingereza pia limesisitiza udharura wa kuimarishwa sheria zilizopo za kukabiliana na vitendo vya chuki, kutekeleza mikakati ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu, na wakati huo huo kutenga rasilimali ili kusaidia wahanga na kuzuia kujikariri matukio kama hayo.