Chama kinachopiga vita Uislamu Uholanzi chapendekeza kifungo jela kwa kubeba Qur'ani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i121362-chama_kinachopiga_vita_uislamu_uholanzi_chapendekeza_kifungo_jela_kwa_kubeba_qur'ani
Katika msimamo wake wa hivi karibuni dhidi ya Uislamu, chama chenye misimamo mikali cha Uholanzi "The Party for Freedom" kimetaka kupitishwa sheria ya kumfunga jela mtu yeyote ambaye ana nakala ya Qur'ani.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Jan 13, 2025 00:03 UTC
  • Chama kinachopiga vita Uislamu Uholanzi chapendekeza kifungo jela kwa kubeba Qur'ani

Katika msimamo wake wa hivi karibuni dhidi ya Uislamu, chama chenye misimamo mikali cha Uholanzi "The Party for Freedom" kimetaka kupitishwa sheria ya kumfunga jela mtu yeyote ambaye ana nakala ya Qur'ani.

Wito wa Chama cha The Party for Freedom cha Uholanzi, kikiongozwa na mwanasiasa mashuhuri kwa kupiga vita Uislamu, Geert Wilders, wa kuandaliwa sheria ya kuwafunga jela miaka mitano watu wanaomiliki nakala za Qur'ani, umelaaniwa na watu wengi.

Licha ya kwamba Chama cha The Party for Freedom cha Uholanzi hakijatoa tamko kuhusiana na pendekezo la kufungwa jela miaka mitano wale wanaomiliki nakala za Qur'ani, mmoja wa viongozi wa muungano wa serikali ya Uholanzi amesisitiza katika mahojiano ya televisheni kwamba pendekezo hilo limesababisha wasiwasi na kumezusha utata katika jamii ya Uholanzi.

Wilders na chama chake hapo awali walikosoa matukio ya Waislamu kuswali katika maeneo ya umma, na kudai kuwa ni ishara ya kutoweka utambulisho wa Uholanzi.

Geert Wilders

Geert Wilders amekuwa katika ulinzi wa polisi wa Uholanzi tangu 2004 kutokana na vitisho vya mara kwa mara na anatumia vibaya majukwaa yake ya vyombo vya habari kushambulia Uislamu na Waislamu.