Seneta wa Marekani anayepinga Iran ahukumiwa kifungo cha miaka 11 jela
Seneta wa Marekani ambaye alikuwa na misimamo mikali dhidi ya Iran amehukumiwa kifungo kwa kupatikana na hatia ya ufisadi na kupokea hongo.
Bob Menendez aliyekuwa seneta wa New Jersey kwa tiketi ya chama cha Democratic amehukumiwa kifungo cha miaka 11 jela kwa makosa ya kula rushwa na hongo, ikiwa ni pamoja na kupokea pesa taslimu, gari aina ya Mercedes Benz na vipande vya dhahabu kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara watatu na serikali ya Misri.
Menendez, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Mahusiano ya Kigeni, alipatikana na hatia mwaka jana kwa makosa 16 kuhusiana na kesi ya rushwa ya muda mrefu, na kumfanya kuwa seneta wa kwanza wa Marekani kushtakiwa na kuhukumiwa kama wakala wa serikali ya kigeni.
Bob Menendez alikuwa seneta mwenye msimamo mkali ambaye alipendekeza kuwekwa vikwazo vikali zaidi dhidi ya Iran na alijulikana kama mtu anayeipiga vita Jamhuri ya Kiislamu.