UNICEF: Mashambulio ya Israel yanaua kila siku watoto 28 Wapalestina Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128458
Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell, ameweka hadharani takwimu za kutisha kuhusu athari za mashambulizi ya kinyama yanayoendelea kufanywa na utawala wa kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.
(last modified 2025-07-18T14:06:34+00:00 )
Jul 18, 2025 05:06 UTC
  • UNICEF: Mashambulio ya Israel yanaua kila siku watoto 28 Wapalestina Ghaza

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell, ameweka hadharani takwimu za kutisha kuhusu athari za mashambulizi ya kinyama yanayoendelea kufanywa na utawala wa kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Bi Russell ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mkurugenzi huyo mtendaji wa UNICEF amethibitisha kuwa zaidi ya watoto 17,000 Wapalestina wameuawa tangu Israel ilipoanzisha vita dhidi ya Ghaza, kwa wastani wa watoto 28 kila siku - sawa na darasa zima.

"Ni kana kwamba tunapoteza darasa zima la wanafunzi kila siku kwa muda wa miaka miwili”, ameeleza afisa huyo wa Unicef.

Bi Russell ameendelea kueleza: "watoto si wahusika wa kisiasa. Hawaanzishi mizozo, na hawana uwezo wa kuizuia. Lakini wanateseka sana, na wanashangaa kwa nini ulimwengu umewatelekeza".

Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher ametahadharisha kuwaa hali ya huduma za afya katika eneo la Ghaza imefikia viwango vya maafa.

Akihutubia kikao hicho cha Baraza la Usalama la UN, Fletcher amesema: "ni hospitali 17 tu kati ya 36 na 63 kati tu ya vituo 170 vya huduma za afya za msingi vinafanya kazi, zote kwa kiwango cha wastani tu, hata kama majeruhi wengi hufika kila siku"…/