Seneta wa Russia: Trump ameangukia kwenye "mtego" wa Ukraine
Kuhusu vita vya Ukraine na misimamo ya karibuni ya Rais wa Marekani, Seneta huyo wa Russia amesema: "Trump ameingia kwenye mtego wa Ukraine.
Akitoa radiamali yake kwa misimamo ya White House Alexey Pushkov ambaye ni Seneta wa Russia ameandika hivi katika ukurasa wake wa Telegram: Rais Donald Trump wa Marekani huko nyuma alikaribia kutumbukia kwenye mtego wa Ukraine, lakini sasa hivi atatumbukia kikamilifu katika mtego huo iwapo hatotekeleza ahadi yake ya kuanza tena kuipatia Kiev misaada ya kijeshi.
Pushkov amesisitiza kuwa: Trump tayari amepiga hatua moja mbele mbali na mtego huo wa Waukraine kwa kuunga mkono mpango wa kutuma silaha na zana za kijeshi za Marekani kwa Kiev. "Hatua moja zaidi inatosha kukamilisha mtego huo; Trump hawezi tena kuhepa," amesemaSeneta wa Russia Alexey Pushkov.
Amesema hali kama hii huko nyuma ilishuhudiwa pia huko Vietnam na Afghanistan. Kuhusu vita vya Ukraine pia, Seneta huyo wa Russia amesema kuwa: Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden aliiingiza Washington katika vita hivyo bila sababu."