Walimwengu waandamana kulaani kuwabakisha na njaa wakazi wa Gaza
Wananchi wa miji mbalimbali ya Ulaya na katrikka mataifa ya Kiarabu wameandamana kupinga siasa za utawala wa kizayuni za njaa dhidi ya watu wa Gaza wakati wa vita vya mauaji ya kimbari vya utawala huo ghasibu vilivyodumu kwa miezi 21.
Berlin, mji mkuu wa Ujerumani, ulishuhudia maandamano ya wafuasi wa Palestina siku ya Ijumaa kupinga siasa za utawala wa Israel za njaa dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Mamia ya waungaji mkono wa Palestina walikusanyika kwenye mtaa wa Sigismund, karibu na ubalozi wa Misri mjini Berlin na Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani. Waandamanaji hao, walileta sahani, masufuria na vijiko na kuvivunja wakati wa maandamano ya kulaani hatua ya utawala wa Israel ya kuzuia misaada ya chakula Gaza na siasa zake za njaa dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
Waandamanaji walibeba bendera za Palestina na mabango yenye kaulimbiu kama vile "Komesha mauaji ya halaiki," "Kunyamaza ni kushiriki katika uhalifu," "Fungua kivuko cha Rafah na uokoe raia," na "Ndiyo kwa mkate, hapana kwa
Katika mji mkuu wa Uingereza, London, hasa mbele ya makao makuu ya serikali huko Downing Street, makumi ya maelfu ya watu waliandamana Ijumaa jioni kuitikia wito wa "Muungano wa Wapalestina nchini Uingereza", wakikataa sera ya kuwabakisha na njaa Wapalestina huko Gaza na kutaka kukomeshwa mara moja mzingiro na mauaji ya kimbari yanayoendelea dhidi ya raia.
Katika nchi za Kiarabu, ikiwa ni pamoja na Morocco, maelfu ya watu walishiriki katika maandamano ya mshikamano na Gaza kwa wiki ya 86 mfululizo, yaliyoandaliwa chini ya kaulimbiu "Hapana kwa njaa, hapana kwa mzingiro, hapana kwa uhusiano wa kawaida na Israel."