Kituo cha silaha za nyuklia cha Uingereza chavujisha mada za radioactive
Mada za radioactive zimeripotiwa kuvuja baharini kutoka katika kituo kinachohifadhi mabomu ya nyuklia ya Uingereza baada ya mabomba ya zamani kupasuka mara kadhaa.
Nyaraka rasmi zinaonyesha kuwa mada za radioactive zimevuja katika eneo la ziwa Loch Lomond. Mada hizo zimetoka katika kituo cha kijeshi cha Coalport magharibi mwa Scotland, ambako mabomu ya nyuklia ya Jeshi la Wanamaji la Uingereza yanahifadhiwa.
Miaka kadhaa iliyopita, vyombo vya habari vya Uingereza viliripoti mara kadhaa kuhusu kuvuja maji ya mionzi kutoka kituo hicho cha nyuklia.
Hivi karibuni pia, ripoti zilieleza kuhusu kuvuja mada za radioactive za tritinium.
Ingawa Shirika la Kulinda Mazingira la Scotland lilitangaza kuwa viwango hivyo vilikuwa chini sana kuweza kuhatarisha afya ya binadamu, matukio hayo yameibua wasiwasi kuhusu usimamizi dhaifu katika mojawapo ya kambi za siri za kijeshi za Uingereza.
Nyaraka zilizokusanywa na Shirika la Kulinda Mazingira ya Scotland (Sepa) ambayo ni taasisi ya serikali inayoshughulikia uchafuzi wa mazingira zinaonyesha kuwa nusu ya vifaa vya kituo hicho vimechaa kwa kiasi kikubwa.