Ufuska Ujerumani: Maambukizi ya magonjwa ya zinaa yaongezeka kwa 460%
https://parstoday.ir/sw/news/world-i131354-ufuska_ujerumani_maambukizi_ya_magonjwa_ya_zinaa_yaongezeka_kwa_460
Mambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs) yanaonekana kuongezeka kwa kiwango cha kuogofya nchini Ujerumani.
(last modified 2025-09-28T12:21:01+00:00 )
Sep 28, 2025 12:21 UTC
  • Ufuska Ujerumani: Maambukizi ya magonjwa ya zinaa yaongezeka kwa 460%

Mambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs) yanaonekana kuongezeka kwa kiwango cha kuogofya nchini Ujerumani.

Idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa zinaa wa kaswende imefikia rekodi mpya ya kutisha nchini Ujerumani, na kufikia kesi 9,519 mnamo 2024 ikilinganishwa na 1,697 tu mwanzoni mwa karne hii, kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni kutoka Taasisi ya Robert Koch (RKI).

Kuenea kwa ugonjwa huo wa zinaa, unaosababishwa na bakteria Treponema pallidum, imeongezeka kwa kasi ya kutisha katika miongo miwili iliyopita. Kesi za magonjwa ya zinaa zimeongezeka kwa asilimia 460 tangu 2001, ripoti ya hivi karibuni ya Taasisi ya Robert Koch inaonyesha.

Baada ya kufikia kesi 3,364 mwaka 2004, idadi hiyo imeendelea kuongezeka, hasa miongoni mwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Kwa mujiibu wa takwimu hizo mpya, wanaojihusisha na vitendo vya mahusiano ya watu wa jinsia moja LGBTQ walichangia idadi kubwa ya maambukizi hayo. Karibu robo tatu ya kesi zilizoripotiwa zinahusishwa na wanachama wa LGBTQ, na data inayoonyesha kuwa hadi nusu ya wagonjwa hawa pia wana virusi vya HIV.

Hivi karibuni pia, takwimu mpya za Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini humo (CDC) zilionyesha kuwa, maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama kisonono, kaswende na klamidia (chlamydia) yameongezeka maradufu miongoni mwa watu wenye umrii wa miaka 55 na zaidi katika kipindi cha miaka 10 baina ya 2012 na 2022.

Si vibaya kuashiria hapa kuwa, maambukizi ya maradhi ya zinaa hususan chlamydia miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 45 na zaidi yaliongezeka kwa asilimia 22 nchini Uingereza mwaka 2022.

Wataalamu wa afya wanasema kuwa, kampeni kubwa ya kushajiisha ndoa na mahusiano ya kishoga ya watu wenye jinsia moja imechangia pakubwa ongezeko la maambukizi ya magonjwa ya zinaa katika nchi za Magharibi.