Bunge la Peru lamuondoa madarakani Rais Dina Boluarte
Rais wa Peru mama Dina Boluarte ameondolewa madarakani kwa kura nyingi za wabunge, kufuatia hoja kadhaa zilizowasilishwa na makundi mbalimbali ya vyama vya siasa bungeni.
"Kutimuliwa kwa rais kumeidhinishwa," ametangaza Spika wa Bunge José Jerí, kufuatia kikao kifupi ambacho Boluarte hakufika, licha ya kutakiwa kushiriki. Boluarte anaweza kujitetea au kuwakilishwa na wakili, amesema Spika wa Bunge José Jerí.
Kwa kumtimua madarakani, angalau wabunge 87 kati ya 122 walioshiriki katika kura hiyo walilazimika kupiga kura kuunga mkono kuondolewa kwake madarakani. Vyama vikuu vya kisiasa katika Bunge viliwasilisha hoja tano za kumtimua madarakani. Uchunguzi wa hoja nne kati hizo zilipitishwa kwa kura nyingi katika Bunge la nchi hiyo.
Hoja hizo zinahimiza "kutokuwa na uwezo wa kudumu wa maadili" wa rais kutekeleza majukumu yake, kulingana na hati zilizosomwa wakati wa ufunguzi wa kikao cha bunge.
Mwanamama Dina Boluarte tayari amekuwa mlengwa wa majaribio kadhaa ya kumfungulia mashtaka, ambayo hakuna hata moja lililofanikiwa. Wakati huu, mchakato huo umefikia hitimisho lake, huku vyama vya mrengo wa kulia na vyama vyenye msimamo mkali vya mrengo wa kulia ambavyo hapo awali vilimuunga mkono vikimtelekeza.
Peru inakabiliwa na kipindi kibaya zaidi cha machafuko ya kisiasa katika historia yake ya kisasa, baada ya kuongozwa na marais sita katika takriban miaka tisa. Baada ya kuingia madarakani baada ya kufutwa kazi kwa Rais Pedro Castillo, huku kukiwa na maandamano yaliyokandamizwa kwa nguvu na kusababisha vifo vya takriban watu 50, Dina Boluarte anakabiliwa na hali ya kutopendwa na watu wengi.