Wananchi wa Korea Kusini waandamana kuunga mkono Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i135328-wananchi_wa_korea_kusini_waandamana_kuunga_mkono_palestina
Raia wa Korea Kusini wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Seoul na kutangaza mshikamano wao na wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-01-10T08:40:53+00:00 )
Jan 10, 2026 08:40 UTC
  • Wananchi wa Korea Kusini waandamana kuunga mkono Palestina
    Wananchi wa Korea Kusini waandamana kuunga mkono Palestina

Raia wa Korea Kusini wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Seoul na kutangaza mshikamano wao na wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Waaandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wametoa mwito wa kupelekwa bila kuzuiizi misaada ya kibinadamu kwa wananchi wa Ukanda wa Gaza wanaokabiliwa na mzingiro wa utawala haramu wa Israel.

Waandamanaji hao mbali na kubeba mabango na maberamu yaliyokuwa na jumbe mbalimbali za kuunga mkono Palestina wametoa mwito wa kushughulikiwa haraka maafa ya kibinadamu yanayolikabili eneo la Ukanda wa Gaza.

Kadhalika waaandamanaji hao wamekosea uzembe wa jamii ya kimataifa na kuzitaka asasi za kimataifa kuchukua hatua za maana na za haraka kukomesha hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda huo.

Wakati huo huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi Wapalestina (UNRWA) limetangaza kuwa vizingiti vilivyowekwa na  jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika njia za kuingia Ukanda wa Gaza vimesababisha kupungua kwa kiwango kikubwa misaada kwa  Wapalestina katika eneo hilo.

Hayo yanajiri wakati ambao Wizara ya Afya ya Palestina imeeleza katika takwimu zake za hivi karibuni kwamba, Wapalestina zaidi ya 71,000 wameuawa shahidi katika vita vya mauaji ya kimbari vilivyoanzishwa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza Oktoba 2023.

Ofisi Kuu ya Takwimu ya Palestina ilisema katika ripoti yake ya kufunga mwaka wa 2025 kwamba, mauaji ya kimbari, watu kulazimishwa kuhama makazi yao, na uharibifu mkubwa wa miundombinu muhimu, yote haya yamesababisha maafa makubwa na ya muda mrefu kwa utulivu wa kijamii, hali ya kiuchumi na kijamii na haki za binadamu katika ardhi za Palestina.