CENTCOM: Wanajeshi wetu waliojeruhiwa katika vita dhidi ya Iran wamefika 290
-
Makao ya CENTCOM
Kamandi Kuu ya jeshi gaidi la Marekani (CENTCOM) imetangaza kuwa karibu wanajeshi 290 wa nchi hiyo wamejeruhiwa katIka vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Idadi ya wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa vitani iliyotolewa wiki iliyopita ilikuwa karibu askari 200 lakini msemaji wa CENTCOM jana usiku alisema kuwa wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa vitani hadi sasa ni karibu 290. Afisa huyu wa Kamandi kuu ya jeshi la Marekani amedai kuwa wanajeshi 255 kati ya 290 waliojeruhiwa wamerudi kazini na 10 wengine wamejeruhiwa vibaya.
Siku kadhaa zilizopita afisa mmoja wa Marekani aliiambia televisheni ya CNN kwamba askari waliojeruhiwa vitani wako mahatuti na kwamba kuna uwezekano wakaaga dunia wakati wowote.
Mbali na hao, wanajeshi wengine 13 wa Marekani wameuliwa vitani. Jenerali Dan Caine Mkuu wa Majeshi ya Marekani awali alikuwa amesema kwamba wanajeshi wengi wa nchi hiyo wamejeruhiwa katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Iran.
Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani imekiri kuhusu kujeruhiwa na kuuawa wanajeshi wa nchi hiyo katika vita dhidi ya Iran katika hali ambayo Tim Kaine Seneta wa chama cha Democratic ametahadharisha kuwa gharama za vita vilivyoanzishwa na Rais Donald Trump zinalipwa na wananchi wa Marekani.
Seneta huyo ameashiria gharama kubwa za vita dhidi ya Iran na kusema: Wanajeshi wa Marekani wanauawa kwa sababu uongozi wa kisiasa wameiacha diplomasia kwa mbinu ya kutisha.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa serikali ya Marekani inachuja na kuficha idadi halisi ya wanajeshi wa nchi hiyo waliouawa hadi sasa katika vita vyake dhidi ya Iran.