Watoto wakimbizi 360 watoweka wakiwa Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i14641-watoto_wakimbizi_360_watoweka_wakiwa_uingereza
Mamia ya watoto wakimbizi wametoweka baada ya kuwasili Uingereza huku kukiwa na wasiwasi kuwa baadhi wanadhalilishwa kingono na wengine wakiwa katika utumwa mamboleo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Sep 04, 2016 23:54 UTC
  • Watoto wakimbizi 360 watoweka wakiwa Uingereza

Mamia ya watoto wakimbizi wametoweka baada ya kuwasili Uingereza huku kukiwa na wasiwasi kuwa baadhi wanadhalilishwa kingono na wengine wakiwa katika utumwa mamboleo.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza imesema haijui ni wapi walipo watoto 320 walioingia nchini humo hivi karibuni.Ripoti hiyo imesema kuna wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama wa watoto hao. Wabunge na wanaharakati wanasema takwimu hizo zinaonyesha kufeli serikali ya Waziri Mkuu Theresa May.

Watetezi wa haki wanasema baadhi ya watoto hao wanatekwa na wasafirishaji binadamu, wengine wakidhalilishwa kingono na baadhi wakifanya watumwa. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watoto 9,287 wameingia Uingereza pasina kuwa na wazazi au walezi wao.

Watoto wakimbizi kutoka Syria

Watoto wengi huwa wanatoroka umasikini, vita, na ukandamizaji katika nchi zao asili. Uchunguzi uliofanywa na Kitengo cha Upelelezi cha Polisi ya Ulaya, Europol, umebaini kuwa, watoto 10,000 wakimbizi wametoweka miaka ya hivi karibuni baada ya kuwasili barani humo.