Sarkozy: Ulaya inaihitajia Russia ili kutatua mgogoro wa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i15556-sarkozy_ulaya_inaihitajia_russia_ili_kutatua_mgogoro_wa_syria
Rais wa zamani wa Ufaransa amesema kuwa Ulaya inapasa kushirikiana na Russia ili kuweza kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 18, 2016 02:55 UTC
  • Sarkozy: Ulaya inaihitajia Russia ili kutatua mgogoro wa Syria

Rais wa zamani wa Ufaransa amesema kuwa Ulaya inapasa kushirikiana na Russia ili kuweza kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria.

Nicolaus Sarkozy Rais wa zamani wa Ufaransa ameashiria nafasi chanya ya Russia katika kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria na kusisitiza kuwa, mustakbali wa Ulaya na Russia unategemea kila upanda na kwamba nchi za Ulaya zinapasa kushirikiana na Moscow kupata ufumbuzi wa kadhia ya Syria. 

Mazungumzo ya Geneva ya kutatua mgogoro wa Syria 

Sarkozy ameongeza kuwa siasa za nchi za Ulaya za  kuiwekea vikwazo Russia ni kosa kubwa na kwamba kuendelea mwenendo huo kunaandaa mazingira ya kuanza vita baridi vipya kati ya Ulaya na Russia. Rais wa zamani wa Ufaransa pia ametaka kuondolewa vikwazo vya Ulaya dhidi ya Russia. Uhusiano kati ya Russia, Umoja wa Ulaya na Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) uliingia dosari katika miaka miwili ya hivi karibuni kutokana na kadhia ya Ukraine. Kwa kufuata kibubusa siasa za Marekani, Umoja wa Ulaya umeamua kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Russia na pia kuwaweka baadhi ya viongozi na raia wa nchi hiyo katika orodha yake ya vikwazo.