Iran na Vietnam zimesaini hati mbili za ushirikiano
https://parstoday.ir/sw/news/world-i16846-iran_na_vietnam_zimesaini_hati_mbili_za_ushirikiano
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Vietnam zimesaini hati mbili za ushirikiano ili kurahisisha mawasiliano kati ya nchi mbili hizi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 06, 2016 04:12 UTC
  • Iran na Vietnam zimesaini hati mbili za ushirikiano

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Vietnam zimesaini hati mbili za ushirikiano ili kurahisisha mawasiliano kati ya nchi mbili hizi.

Hati mbili hizo zimesainiwa leo asubuhi huko Hanoi mwishoni mwa mazungumzo ya pamoja ya jumbe za ngazi za juu za Iran na Vietman kwa kuhudhuriwa na Rais Hassan Rouhani wa Iran na mwenzake wa Vietnam Tran Dai Quang.

Marais wa Iran na Vietnam wakishhudia hati za ushirikiano zikisainiwa

Hati ya pili ya ushirikiano kati ya nchi mbili hizi imesainiwa kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Wizara ya Mawasiliano na Habari ya Vietnam. Hati hii imesainiwa ili kushirikiana katika nyanja ya mawasiliano na teknolojia ya habari. Marais wa Iran na Vietnam walikuwa na kikao na waandishi wa habari baada ya kusainiwa hati mbili za ushirikiano.