Wamarekani wenye hasira waandamana kuwapinga Clinton, Trump
Wananchi wenye hasira wa Marekani wamefanya maandamano katika mitaa ya Washington DC kuwapinga wagombea wawili wa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
Maandamano hayo ni sehemu ya maandamano ya nne ya kimataifa ya kila mwaka maarufu kwa maandamano ya milioni ya watu walioziba nyuso zao. Maandamano hayo huitishwa kila mwaka na kundi la wadukuzi linalojulikana kwa jina la Anonymous.
Wakazi wa Washington DC wamemiminika kwenye barabara za mji huo kulalamikia mfumo wa kiidara na hali mbaya ya kisiasa iliyoko Marekani hivi sasa na pia kampeni za uchaguzi za Hillary Clinton na Donald Trump, wagombea wa urais wa vyama vya Democrat na Republican.
Maandamano hayo yaliyoanza katikati ya mji wa Washington DC yameelekea kwenye majengo ya serikali na katika ofisi za polisi ya FBI pamoja na hoteli ya Donald Trump. Watu kadhaa wametiwa nguvu na polisi wakati wa maandamano hayo.
Televisheni ya Press TV imetangaza habari hiyo na kuonesha waandamanaji waliokuwa wamefunika nyuso zao wakiingia katika hoteli ya Donald Trump jijini Washington wakipiga nara za kukataa misimamo ya Trump katika kampeni zake za uchaguzi. Waandamanaji hao wamelalamikia pia siasa na kashfa za mgombea mwengine wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrat, Hillary Clinton na kusema kuwa, wagombea wote hao wawili ni madhara kwa Marekani.