Russia: Madai kuwa Putin aliingilia uchaguzi wa Marekani ni 'dhihaka'
https://parstoday.ir/sw/news/world-i21514-russia_madai_kuwa_putin_aliingilia_uchaguzi_wa_marekani_ni_'dhihaka'
Msemaji wa Ikulu ya Russia (Kremlin) amesema madai yanayoenezwa na vyombo vya habari kuwa Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo aliingilia uchaguzi wa Marekani ni 'dhihaka' na madai ya upuuzi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 16, 2016 04:46 UTC
  • Russia: Madai kuwa Putin aliingilia uchaguzi wa Marekani ni 'dhihaka'

Msemaji wa Ikulu ya Russia (Kremlin) amesema madai yanayoenezwa na vyombo vya habari kuwa Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo aliingilia uchaguzi wa Marekani ni 'dhihaka' na madai ya upuuzi.

Dmitry Peskov amesema madai hayo yanayoenezwa na vyombo vya habari kama NBC kuwa Rais Putin alihusika moja kwa moja yeye binafsi katika kuchakachua matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Marekani haya msingi na ya kichekesho.

Rais Vladimir Putin wa Russia

Kuhusiana na suala hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Ryabkov amesema Moscow ilikuwa na mawasiliano na baadhi ya watu wa karibu na Donald Trump wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais wa Marekani na kwamba mawasiliano hayo yangali yanaendelea. 

Msemaji wa Kremlin amesema mtazamo wa Rais wa Russia na Rais mteule wa Marekani katika sera za nje unafanana na kwamba mshabihiano huo unaweza kuwa msingi imara wa kuanzishia mazungumzo ya dhati kati ya Moscow na Washington.

Rais Barack Obama ambaye karibuni hivi atakabidhi madaraka kwa Trump, ametishia kumuwajibisha Putin, kwa kuingilia uchaguzi huo wa rais wa Marekani, kwa maslahi ya Trump.

Trump na Clinton