Le Monde: Putin Shakhsia mashuhuri wa mwaka 2016
https://parstoday.ir/sw/news/world-i22528-le_monde_putin_shakhsia_mashuhuri_wa_mwaka_2016
Gazeti la Ufaransa la Le Monde limemtangaza Rais Vladimir Putin wa Russia kuwa ndiye shakhsia na mtu mashuhuri zaidi katika mwaka huu wa 2016.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 31, 2016 23:30 UTC
  • Le Monde: Putin Shakhsia mashuhuri wa mwaka 2016

Gazeti la Ufaransa la Le Monde limemtangaza Rais Vladimir Putin wa Russia kuwa ndiye shakhsia na mtu mashuhuri zaidi katika mwaka huu wa 2016.

Le Monde limeandika kuwa, licha ya mjada mkubwa uliohusu kuchaguziliwa kwa Donald Trump kuwa Rais mpya wa Marekani, Vladimir Putin ndiye mtu mashuhuri zaidi katika mwaka huu wa 2016.

Le Monde limeongeza kuwa, katika kipindi chote cha miaka 16 ya uongozi wake, Putin ameweza kuwa na nafasi muhimu nchini Russia na ulimwenguni.

Vladimir Putin

Gazeti hilo limeandika kuwa, licha ya mivutano iliyopo baina ya Rais wa Rusia na Umoja wa Ulaya lakini Putin ameweza kuimarisha uhusiano wa kistratijia na vyama na wanasiasa wakubwa wenye mielekeo kama yake  barani Ulaya. Le Monde limeongeza katika tahariri yake kwamba, ushawishi wa Rusia katika duru za kiutamaduni na kisiasa barani Ulaya umeongeza kwa kiwango kikubwa katika mwaka huu wa 2016.

Barack Obama na Vladimir Pitin

Uhusiano wa Russia na Umoja wa Ulaya na Marekani ulivurugika baada ya machafuko ya ndani nchini Ukraine na kuwa mbaya zaidi baada ya Russia kuliunganisha eneo la Crimea na ardhi yake.