Maaskofu wa Marekani watuhumiwa kuficha ufuska wa makasisi wa kuwanajisi watoto
(last modified Thu, 03 Mar 2016 07:52:58 GMT )
Mar 03, 2016 07:52 UTC
  • Maaskofu wa Marekani watuhumiwa kuficha ufuska wa makasisi wa kuwanajisi watoto

Maaskofu wawili wa Marekani wamepatikana na hatia kuwa walificha vitendo viovu vya makaksi wa Kikatoliki vya kuwanajisi watoto wadogo.

Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa jana, mahakama moja ya Marekani imewapata na hatia maaskofu hao wawili kwa kuficha uhalifu wa mkasisi 50 wa Kikatoliki waliowanajisi mamia ya watoto wadogo katika kipindi cha miongo minne huko katika jimbo la Pennsylvania.

Faili la mahakama hiyo lina ripoti yenye kurasa 147 inayothibitisha kuwa, maaskofu James Hakan na Joseph Adamack walikuwa na habari za kesi nyingi za vitendo viovu vya makasisi vya kuwanajisiwa watoto wadogo lakini walificha uovu huo ili makasisi hao wa Kikatoliki wasikamatwe na polisi.

Mwanasheria Mkuu wa Pennsylvania, Kathleen Kane ambaye amechapisha ripoti hiyo amesema mwenendo wa maaskofu hao wawili umehatarisha maisha ya maelfu ya watoto na kuwapa ruhusa wahalifu huo kuwanajisi watoto wengi zaidi. Mwanasheria Mkuu wa Pennsylvania anasema watoto hao wamenajisiwa katika eneo ambalo lilipaswa kuwadhaminia usalama zaidi.