Mbunge wa Matuga, Kenya: Wanaadamu wote waunge mkono uhuru wa Palestina
Mkutano wa Sita wa Kimataifa wa Kuunga Mkono Intifadha ya Palestina ulimalizika Jumatano hapa Tehran, ambapo kulikuwa wa washiriki zaidi ya 700 kutoka 80.
Mkutano ulimalizika kwa kusisitizia udharura wa kulindwa kadhia ya Palestina ambayo ni kipaumbele cha kwanza cha nchi ulimwengu wa Kiislamu na za Kiarabu na ndilo zingatio kuu la fikra za walio wengi duniani.
Kati ya walioshiriki katika mkutano huo alikuwa ni Mhe. Hassan Mwanyoha Mbunge wa Matuga eneo la Pwani nchini Kenya ambaye alizungumza na mwandishi wa Radio Tehran Mubarak Henia baada ya mkutano na kusema Kadhia ya Palestina si ya Waislamu tu bali uhuru wa Palestina unapaswa kutetewa na walimwengu wote. Sikiliza mahojiano kupata tathmini yake kamili ya mkutano huo