Mar 13, 2017 07:06 UTC
  • Watu 25 wauawa na kujeruhiwa usiku mmoja nchini Marekani

Watu 10 wameuawa na 15 wengine wamejeruhiwa katika mashambulizi ya usiku mmoja yaliyotokea jana usiku katika kona mbalimbali za Marekani.

Shirika la habari la IRIB limetagaza kuwa, mashambulizi yaliyotokea katika mji wa Cincinnati wa jimbo la Ohio na mji wa Atlanta wa jimbo la Georgia yamepelekea watu watano kujeruhiwa.

Mashambulizi ya jana usiku yaliyotokea kwenye mji wa Dayton jimbo la Ohio na mji wa Chicago wa jimbo la Illinois yameua watu wawili na kujeruhi wengine wawili.

Watu wengine wawili walijeruhiwa jana usiku katika mashambulizi yaliyotokea kwenye mji wa Cleveland huko Ohio na Tulsa katika jimbo la Oklahoma.

Rais Donald Trump wa Marekani mwenye chuki na wageni hususan Waislamu

 

Watu wengine watano waliuawa jana usiku nchini Marekani katika mashambulizi yaliyotokea kwenye majimbo ya Kentucky na Carolina Kaskazini.

Kona zote za Marekani ziliendelea kushuhudia mashambulizi ya silaha za moto jana usiku yakiwemo majimbo ya Virginia, Maryland, California, Alabama na Hawaii.

Mashambulizi ya kiholela na ya chuki yameongezeka nchini Marekani tangu alipoingia madarakani Rais Danald Trump anayewachukia wageni hususan Waislamu.

Tags