Wasomi wengi duniani wanaamini Iran ina uwezo mkubwa wa kijeshi, kisiasa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i27520-wasomi_wengi_duniani_wanaamini_iran_ina_uwezo_mkubwa_wa_kijeshi_kisiasa
Aghalabu ya wasomi wa nchi mbali mbali duniani wanaamini kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo mkubwa wa kijeshi na ina taathira katika uga wa kimataifa.
(last modified 2026-07-03T11:45:53+00:00 )
Apr 09, 2017 09:42 UTC
  • Wasomi wengi duniani wanaamini Iran ina uwezo mkubwa wa kijeshi, kisiasa

Aghalabu ya wasomi wa nchi mbali mbali duniani wanaamini kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo mkubwa wa kijeshi na ina taathira katika uga wa kimataifa.

Kwa mujibu wa tovuti ya usnews.com Chuo Kikuu cha Pennsylvania kimefanya uchunguzi wa maoni hivi karibuni ambapo wasomi kutoka maeneo ya Asia, Ulaya, Amerika, Afrika, Mashariki ya Kati wamehojiwa kuhusu uwezo wa Iran katika sekta za kijeshi na ulinzi.  Asilimia 77 ya waliohoijiwa wamesema wanaamini kuwa Iran ina uwezo mkubwa wa kijeshi.

Aidha asilimia 44 ya wasomi hao wa dunia wameitaja Iran kuwa nchi yenye taathira katika uga wa siasa za kimataifa.

Kombora la Balistiki la Emad lililotengenezwa na wataalamu wa kijeshi nchini Iran

Aghalabu ya walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni wanasema urasimu usiohitajika ni moja ya sababu zilizopelekea kudhoofika Iran kibiashara huku asilimia 20 miongoni mwa wasomi hao wakisema gharama za chini za uzalishaji bidhaa nchini Iran ni fursa nzuri ya kuwekeza katika nchi hii.