Ujerumani: Tulitamani kumpindua Bashar al Assad lakini tumeshindwa vibaya
-
Peter Witting, balozi wa Ujerumani nchini Marekani
Balozi wa Ujerumani mjini Washington, Marekani sambamba na kukiri kwamba nchi za Magharibi zinawasaidia magaidi kufanya jinai nchini Syria, amesema kwamba, tulikuwa na hamu kubwa ya kuipindua serikali ya Bashar al Assad lakini tumeshindhwa vibaya sana.
Shirika la habari la Tasnim limemnukuu Peter Witting, balozi wa Ujerumani nchini Marekani akisema hayo jana Jumatatu mjini Washington na kuongeza kuwa, juhudi za nchi za Magharibi za kumpindua Bashar al Asad zimeshindwa na hilo ni pigo kubwa kwa kile alichodai eti ni jamii ya kimataifa.
Amesema, ni jambo lisilo na shaka kwamba yeye pamoja na balozi wa Uingereza nchini Marekani walikuweko katika Baraza la Usalama la Umoja wa

Mataifa wakati yalipoanza machafuko nchini Syria na walitamani kwamba machafuko hayo yawe na maana ya siku za mwisho za serikali ya Bashar al Assad, lakini wameshindwa vibaya.
Balozi wa Ujerumaini nchini Marekani ameongeza kuwa, damu bado inaendelea kumwagika nchini Syria na hadi hivi sasa Bashar al Assad ni Rais wa Syria na ana mwakilishi katika Umoja wa Mataifa.
Amesema: "Hili linaweza kuwa ni jambo la kusikitisha, lakini ukweli ni kwamba, licha ya kufanya juhudi kubwa za kisiasa na kidiplomasia, tumeshindwa kubadilisha chochote."

Pia amesema, kuna uwezekano nchi zilizoungana kutaka kumpindua Bashar al Assad zimepata pigo kubwa katika historia na zimesababisha maafa ya kutisha kwa jamii ya mwanadamu.
Balozi huyo wa Ujerumaini mjini Washington ameongeza kuwa: "Ninayasema haya kwa masikitiko, lakini huu ndio ukweli wenyewe na inabidi tukubaliane na ukweli huo."