Dec 26, 2017 07:39 UTC
  • Ripoti: Uuzaji wa mihadarati Marekani kuongezeka kwa asilimia 45

Uuzaji 'halali' wa dawa ya kulevya aina ya bangi umeongezeka kwa asilimia 30 mwaka huu nchini Marekani, na mauzo hayo yanatazamiwa kuongezeka hadi asilimia 45 kufikia mwaka ujao 2018.

Kwa mujibu wa utafiti wa gazeti la Marijuana Business Daily, fedha zinazotokana na uuzaji wa dawa hiyo ya kulevya zimefikia kiwango cha juu zaidi katika historia, cha dola bilioni 17 za Marekani.

Ripoti hiyo inasema kuwa,  majimbo 23 ya Marekani yameruhusu utumiaji wa dawa ya kulevya aina ya bangi, hata katika masuala yasiyo ya kitiba.

Inaelezwa kuwa, takribani asilimia 70 ya wananchi wa Marekani wametumia bangi japo mara moja katika kipindi cha maisha yao. 

 

Kwa mujibu wa utafiti wa maoni wa Gall Up uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu, asilimia 64 ya Marekani wanataka kuona bangi 'ikihahalishwa' kote nchini.

Uruguay ndiyo nchi pekee duniani iliyohalalisha kikamilifu utumiaji wa bangi au marijuana. Kilimo cha dawa hiyo ya kulevya nchini humo kiliruhusiwa mwaka 2014 huku uuzaji wake ukiidhinishwa rasmi Julai mwaka huu.

Canada inatazamiwa kufuata mkondo huo kufikia Julai mwaka ujao 2018.

Tags