Kiongozi wa eneo la Catalani atiwa mbaroni Ujerumani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i42174-kiongozi_wa_eneo_la_catalani_atiwa_mbaroni_ujerumani
Kiongozi wa zamani wa eneo la Catalani linalotaka kujitenga na Uhispania, Carles Puigdemont ametiwa mbaroni leo na polisi nchini Ujerumani kufuatia waranti wa kimataifa uliotolewa na Uhispania.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Mar 25, 2018 09:50 UTC
  • Kiongozi wa eneo la Catalani atiwa mbaroni Ujerumani

Kiongozi wa zamani wa eneo la Catalani linalotaka kujitenga na Uhispania, Carles Puigdemont ametiwa mbaroni leo na polisi nchini Ujerumani kufuatia waranti wa kimataifa uliotolewa na Uhispania.

Puigdemont aliwasili Ujerumani akitokea Denmark baada ya kuondoka Finlad siku ya Ijumaa ambapo ilionekana kuwa polisi wanaweza kumtia nguvuni nchini humo na kuanzisha mchakato wa kumrejesha huko Uhispania kama ilivyoombwa na nchi hiyo.

Wakili anayemtetea kiongozi huyo wa eneo la Catalani nchini Uhispania Jaume Alonso-Cuevillas hakueleza wazi mahali anakoshikiliwa Puigdemont huko Ujerumani. Amesema kwamba Puigdemont kiongozi wa zamani wa eneo la Catalani alikuwa akielekea Ubelgiji ambako amekuwa akiishi uhamishoni tangu mwaka jana.

Maandamano ya wanaotaka eneo la Catalonia lijitenge na Uhispania

Puigdemont anakabiliwa na kifungo cha jela huko Uhispania cha hadi miaka 25 kwa makossa ya kufanya uasi na kuandaa kura ya maoni kinyume cha sheria iliyopelekea kutangazwa kuwa huru kwa upande mmoja eneo la Catalani mwezi Oktoba mwaka jana.