Trump adai askari wa Marekani wataondoka Syria hivi karibuni
https://parstoday.ir/sw/news/world-i42384-trump_adai_askari_wa_marekani_wataondoka_syria_hivi_karibuni
Rais Donald Trump wa Marekani amedai kuwa askari wa nchi hiyo wataondoka katika ardhi ya Syria hivi karibuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 29, 2018 22:31 UTC
  • Trump adai askari wa Marekani wataondoka Syria hivi karibuni

Rais Donald Trump wa Marekani amedai kuwa askari wa nchi hiyo wataondoka katika ardhi ya Syria hivi karibuni.

Trump ambaye alikuwa akihutubia mkutano katika jimbo la Ohio amesema kuwa: "Karibuni hivi askari wa Marekani wataondoka nchini Syria." Amesema askari wa Marekani wanapaswa kurejea nchini kwao na kuongeza kuwa, Marekani imetumia dola bilioni elfu saba katika eneo la Mashariki ya Kati lakini haikupata chochote. 

Trump pia amezikosoa serikali za marais waliomtangulia wa Marekani na kusema: "Hali ya sasa ya Marekani inashabihiana sana na ya nchi za ulimwengu wa tatu na suala hili linatia aibu." 

Wakati huo huo Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Heather Nauert amesema kuwa, hana habari yoyote kuhusu mpango wa kuondoka askari wa nchi hiyo katika ardhi ya Syria.

Heather Nauert

Madai hayo ya Rais wa Marekani kuhusu suala la kuondoka askari wa nchi hiyo huko Syria na ukosoaji wake dhidi ya kuwepo vikosi vya nchi hiyo katika Mashariki ya Kati yametolewa siku kadhaa tu baada kiongozi huyo kuafiki suala la kuongezwa idadi ya askari wa Marekani nchini Afghanistan.