Sisitizo la Katibu Mkuu wa UN la kuwepo umoja huko Syria
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa kuwepo umoja na uthabiti nchini Syria ni jambo lenye udharura.
Antonio Guterres alisema jana katika kikao kuhusu Syria mjini Brussels Ubelgiji kuwa haifai mgogoro wa Syria utatuliwe kwa njia ya kijeshi na kwamba nchi hiyo haipasi kugawanywa vipande vipande. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliongeza kuwa raia wa Syria zaidi ya milioni 13 wanaishi katika mazingira magumu na wengine milioni sita na nusu wanaishi nje ya nchi hiyo.
Guterres alibainisha kuwa Syria inapasa kuanza kupokea tena misaada ya kifedha ambapo hadi kufikia sasa Umoja wa Mataifa tayari umepokea asilimia 27 ya fedha zinazohitajika kuwasaidia raia wa Syria. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kufikiwa mapatano kuhusu ufumbuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Syria na kurejea nchini wakimbizi na kusisitiza kuwa hakuna njia yoyote ya ufumbuzi wa kijeshi kwa mgogoro wa nchi hiyo.
Kikao cha pamoja kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa kilifanyika jana mini Brussels Ubelgiji lengo likiwa ni kuchunguza mgogoro wa Syria.