Italia kutonunua tena ndege za kivita za F-35 kutoka Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46618-italia_kutonunua_tena_ndege_za_kivita_za_f_35_kutoka_marekani
Katika kile kinachoonekana ni mgogoro katika uhusiano wa kijeshi wa Rome na Washington, Wizara ya Ulinzi ya Italia imesema haitanunua tena ndege za kivita aina ya F-35 za Marekani.
(last modified 2025-10-20T07:03:11+00:00 )
Jul 07, 2018 08:01 UTC
  • Italia kutonunua tena ndege za kivita za F-35 kutoka Marekani

Katika kile kinachoonekana ni mgogoro katika uhusiano wa kijeshi wa Rome na Washington, Wizara ya Ulinzi ya Italia imesema haitanunua tena ndege za kivita aina ya F-35 za Marekani.

Waziri wa Ulinzi wa Italia, Elisabetta Trenta amesema serikali ya nchi hiyo imesitisha mpango wowote wa siku zijazo wa kununua ndege hizo za kijeshi za Marekani, na kuongeza kwamba itaangalia upya makubaliano yaliyopita ya ununuzi huo.

Amesema serikali ya Rome itatizama upya makubaliano ya mwaka 2012 ya kununua ndege za kivita za F-35A zipazo 60 na 30 za F-35B.

Ndege ya kivita ya F-35

Waziri wa Ulinzi wa Italia amesema kuwa, "Hatununui tena ndege za kivita za Lockheed Martin Corp F-35 kutoka Marekani. Takriban pauni bilioni 14 za ununuzi huo zinaweza kutumiwa kuimarisha hali ya maisha na uchumi wetu unaosuasua."

Mwaka 2012, Italia ilipunguza idadi ya ndege za kijeshi za F-35 ilizotaka kununua kutoka Marekani, kutoka 135 hadi 90.