27 wapoteza maisha katika mafuriko Japan, makumi ya wengine watoweka
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46630-27_wapoteza_maisha_katika_mafuriko_japan_makumi_ya_wengine_watoweka
Watu wasiopungua 27 wamepoteza maisha, watano wakiwa mahututi na wengine 47 hawajulikani waliko baada ya mvua kali kunyesha magharibi na katikati mwa Japan na kusababisha mafuriko.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 08, 2018 02:25 UTC
  • 27 wapoteza maisha katika mafuriko Japan, makumi ya wengine watoweka

Watu wasiopungua 27 wamepoteza maisha, watano wakiwa mahututi na wengine 47 hawajulikani waliko baada ya mvua kali kunyesha magharibi na katikati mwa Japan na kusababisha mafuriko.

Kwa mujibu wa Televisehani ya Taifa, NHK, zaidi ya Wajapani milioni 1.6 wamelazimika kuhama makazi yao kutokana na mafuruko.

Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Japan imetahadharisha kuwa majimbo manne katika kisiwa kikuu cha nchi hiyo cha cha Honshu yatakumbwa na mvua zisizo za kawaida ambazo zimetajwa kuwa za kihistoria.

Katika mji wa Motoyama ulio katika kisiwa cha Shikokou milimita 583 za mvua zimenesha kuanzia Ijumaa hadi Jumamosi asubuhi. 

Siku ya Jumamosi watu milioni 1.6 waliamuriwa kuondoka katika makao yao kwa hofu ya kuenea mafuriko na maporomoko ya ardhi huku watu wengine milioni 3.1 wakishauriwa kuondoka. 

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 59 aliyekuwa akisafisha mabomba ya majitaka alisombwa na maji na baadaye alikutwa akiwa amefariki katika mkoa wa Hyogo. Mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 59 na mwanamke mwenye umri wa miaka 52 nao walisombwa na maji kufuatia mito kufurika katika mikoa mingine.

Barabara iliyoharibiwa na mafuriko nchini Japan huko  Aki, katika jimbo la Hiroshima. July 7 2018

Na katika Mkoa wa Hiroshima mwanaume mwenye miaka ya 60 alithibitishwa kufariki baada ya maporomoko ya ardhi kukumba nyumba yake.

Miongoni mwa watu wasiojulikana mahali walipo, wapo waliosombwa na maji kwenye mito au mifereji mikubwa ya maji. Idadi kubwa ya watu wengine bado hawajaonekana baada ya maporomoko ya ardhi kukumba nyumba zao.