Aziz Ahmed Fanus: Saudia inalinda maslahi ya Marekani nchini Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46808-aziz_ahmed_fanus_saudia_inalinda_maslahi_ya_marekani_nchini_afghanistan
Mtaalamu wa masuala ya kisiasa na kieneo wa nchini Afghanistan ambaye pia ni muhadhiri katika Chuo Kikuu cha mjini Kabul, mji mkuu wa nchi hiyo amesema kuwa, Saudi Arabia inalinda kikamilifu maslahi na malengo ya Marekani nchini Afghanistan.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 16, 2018 04:16 UTC
  • Aziz Ahmed Fanus: Saudia inalinda maslahi ya Marekani nchini Afghanistan

Mtaalamu wa masuala ya kisiasa na kieneo wa nchini Afghanistan ambaye pia ni muhadhiri katika Chuo Kikuu cha mjini Kabul, mji mkuu wa nchi hiyo amesema kuwa, Saudi Arabia inalinda kikamilifu maslahi na malengo ya Marekani nchini Afghanistan.

Aziz Ahmed Fanus, ameyasema hayo katika mahojiano na Redio Tehran ambapo sambamba na kuashiria kikao cha wiki iliyopita cha maulama wa baadhi ya nchi za Kiislamu kilichofanyika mjini Jeddah, Saudi Arabia kwa ajili ya kuchunguza masuala ya usalama nchini Afghanistan, amesema kuwa kidhahiri Wasaudi wamekuwa wakijionyesha kwamba wanafuatilia kwa uchanya mambo yanayoendelea Afghanistan. Amesisitiza kwamba katika uhalisia wa mambo, Wasaudi kamwe hawajawahi kuwa na irada ya kudumisha usalama na amani nchini humo.

Pande tatu za Saudia, Marekani na Israel ambazo zinapanga njama pamoja

Aziz Ahmed Fanus amebainisha kwamba Saudia ni moja ya washirika wa kistratijia wa Marekani na ni kwa ajili hiyo ndio katika kufuatilia maslahi yake nchini Afghanistan, inatekeleza mipango ya Marekani. Mtaalamu huyo wa masuala ya kisiasa na kieneo wa nchini Afghanistan amekadhibisha madai ya baadhi ya viongozi wa kikabila juu ya kuwepo tofauti za kikabila nchini Afghanistan na kuongeza kwamba siku zote raia wa nchi hiyo wamekuwa na maslahi ya pamoja kama ambavyo hawana tofauti zozote kati yao. Amesema kwamba, madai ya viongozi hao wa kikabila yanatolewa kwa lengo la kudhamini maslahi yao binafsi na si kwa ajili ya raia wa kawaida. Amesisitiza kwamba suala la tofauti za kikabila liliwahi kuibuliwa na Marekani na Pakistan nchini Afghanistan na kwamba vita vinavyoendelea hivi sasa nchini humo ni vita vya madola yenye nguvu duniani.