Mar 14, 2019 14:30 UTC
  • Cuba: Miamala ya Marekani dhidi ya Venezuela imetoka kwa Manazi

Rais Miguel Díaz-Canel wa Cuba amekosoa vikali uingiliaji wa kivamizi wa Marekani nchini Venezuela na kusema kuwa, vitendo hivyo vimetoka kwa Manazi wa Ujerumani.

Rais Díaz-Canel amesema kuwa uvamizi na uingiliaji wa Washington dhidi ya wananchi na serikali ya Venezuela umepata ilhamu kutoka kwa Manazi. Kadhalika rais wa Cuba amesema kuwa, hakuna mtu mwenye shaka kwamba kuharibiwa vyanzo vya kuzalisha umeme nchini Venezuela kumefanywa na Marekani. Sambamba na ukosoaji huo wa Rais Miguel Díaz-Canel, faili la pili la uchunguzi dhidi ya Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani aliyejitangaza kuwa rais wa Venezuela pamoja na watu wake wa karibu la tuhuma za kuhusika katika uharibifu wa mtandao wa umeme ndani ya nchi hiyo kupitia msaada wa Marekani, limefunguliwa katika mahakama kuu.

Mitambo ya umeme ambayo imeshambuliwa na Marekani

Katika uwanja huo Tarek William Saab, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Venezuela amesema kuwa baadhi ya jumbe za Twitter za Guaidó zinafaa kuwa vielelezo na ushahidi unaoonyesha kwamba mwasiasa huyo ambaye anaungwa mkono na Marekani na nchi za Magharibi, amehusika katika kuongoza hatua za uharibifu wa mitandao ya umeme nchini Venezuela. Kabla ya hapo pia mwezi Julai mwaka jana, Juan Guaidó alishtakiwa kwa kuhusika na njama za kuharibu mtandao wa umeme nchini Venezuela. Kuhusiana na suala hilo, serikali ya China kupitia msemaji wa serikali ya nchi hiyo Lu Kang, imesema kuwa, ipo tayari kusaidia kuondoa matatizo ya kukatwa mtandao wa umeme nchini Venezuela.

Tags