Mar 16, 2019 14:39 UTC
  • CAIR: Trump ndie chanzo cha hujuma za kigaidi misikitini New Zealand

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limesema sera za Rais Donald Trump zimechangia kuchochea hujuma za kigaidi zilizojiri katika misikiti miwili nchini New Zealand Ijumaa na kupelekea Waislamu 49 kuuawa.

Katika taarifa Mkurugenzi Mtendaji wa CAR Nihad Awad amemtumia Trump ujumbe wa moja kwa moja kufuatia ugaidi huo dhidi ya Waislamu nchini New Zealand na kumtaka alaani vikali hujuma hiyo. Awad amemuonya Trump kuwa vitendo vyake vinaathiri vibaya maisha ya watu wasio na hatia Marekani na duniani.  Amemfahamisha Trump kuwa hujuma hiyo ya New Zealand haikuwa jinai ya chuki tu bali hujuma ya kigaidi ya mzungu anayejiona kuwa bora zaidi ya wengine.

Gaidi mwenye umri wa miaka 28 kwa jina Brenton Tarrant raia wa Australia ambaye amehusika na shambulizi dhidi ya msikiti mmoja kati ya miwili iliyoshambuliwa mjini Christchurch nchini New Zealand amekuwa akijitangaza kuwa ni mfuasi wa sera za Rais Donald Trump wa Marekani.

Kijana huyo mwenye chuki za kidini zinazoshabihiana na za Trump aliyarusha hewani mubashara mauaji hayo ya kinyama aliyoyafanya katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook.

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) Nihad Awad

Katika manifesto yake aliyoichapisha kwenye kurasa 87, gaidi huyo ametaja sababu kadha wa kadha za kuhalalisha chuki zake dhidi ya Uislamu, Waislamu na wahamiaji.

Nihad amemfahamisha Trump kuwa wakati wa kampenzi zake za kuwania urais, chuki dhidi ya Uislamu iliongezeka duniani ambapo kumeshuhudiwa ongezeko la hujuma dhidi ya Waislamu wasio na hatia na misikiti.

 

Tags