Venezuela: Mustakbali wa Trump na Pence upo hatarini
(last modified Sat, 23 Mar 2019 14:09:52 GMT )
Mar 23, 2019 14:09 UTC
  • Venezuela: Mustakbali wa Trump na Pence upo hatarini

Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela amesisitizia umuhimu wa kuondolewa madarakani Rais Donald Trump wa Marekani na Mike Pence, Makamu wake wa Rais.

Jorge Arreaza ameyasema hayo akijibu matamshi ya Mike Pence aliyoyatoa kuwalenga viongozi wa Venezuela ambapo Arreaza amesema kuwa, Trump na makamu wake wa rais wanatakiwa kuzingatia mustakbali wa kibinaadamu. Hivi karibuni, Mike Pence na katika mwendelezo wa kuingilia masuala ya ndani ya Venezuela alisambaza makala kupitia jarida moja la Kimarekani akidai kwamba, Rais Nicolás Maduro wa Venezuela anatakiwa kuondoka madarakani kwa ajili ya mustakabali wa nchi hiyo. Akijibu matamshi hayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter amesema kuwa: "Ni suala la dharura na haraka kwamba! Trump na Pence waondoke madarakani." 

Jorge Arreaza, Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela 

Mgogoro kati ya Marekani na Venezuela ulishtadi baada ya Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani wa Venezuela na anayeungwa mkono na Trump na washirika wa Washington kujitangaza kuwa rais wa nchi hiyo, hatua ambayo ni kinyume na sheria na katiba ya Venezuela. Hii ni katika hali ambayo raia na jeshi la nchi hiyo wameendelea kumuunga mkono Rais Nicolás Maduro. 

Tags