Korea Kaskazini yafanyia majaribio kombora jipya la balestiki
(last modified Thu, 18 Apr 2019 13:32:29 GMT )
Apr 18, 2019 13:32 UTC
  • Korea Kaskazini yafanyia majaribio kombora jipya la balestiki

Serikali ya Korea Kaskazini imefanyia majaribio kombora jipya la balestiki.

Shirika la Habari la Korea Kaskazini KCNA limesema kuwa, majaribio hayo ya kombora la balestiki erevu yalifanyika Jumatano ya jana. Katika majaribio hayo alikuwepo Kim Jong-un, Kiongozi wa nchi hiyo. Majaribio hayo ya kombora jipya ya Korea Kaskazini ni ya kwanza tangu kujiri kikao cha mwisho cha mazungumzo kati ya Kim Jong-un na Rais Donald Trump wa Marekani mjini Hanoi, Vietnam hapo tarehe 28 Februari mwaka huu, mazungumzo ambayo yalivunjika. Kabla ya hapo viongozi hao walikutana nchini Singapore mwezi Juni mwaka jana ambapo walifikia makubaliano ambayo hata hivyo Marekani ilikataa kuyatekeleza. Serikali ya Pyongyang inadai kwamba kupenda makubwa kwa Trump katika mazungumzo ya duru ya pili mjini Hanoi, ndiyo ilikuwa sababu ya kuvunjika kwake.

Kufanya mazungumzo na Trump, hakukuisaidia Korea Kaskazini

Hatua za hivi karibuni za vikwazo vya Marekani dhidi ya Korea Kaskazini, hatua ya Korea Kusini kununua silaha mpya na pia duru mpya ya maneva za kijeshi kati ya Marekani na washirika wake katika eneo la Rasi ya Korea, zimeifanya serikali ya Pyongyang kutangaza kwamba itaanzisha upya majaribio yake ya makombora. Licha ya Korea Kaskazini kuonyesha nia njema kwa lengo la kutatua mzozo wa nyuklia katika eneo, lakini Marekani haikutekeleza makubaliano iliyoyafikia na nchi hiyo, kama ambavyo imeendelea kuiwekea vikwazo na mashinikizo nchi hiyo ya Asia.

Tags