Trump amdhalilisha mfalme wa Saudi Arabia kwa mara ya kumi + Video
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53420-trump_amdhalilisha_mfalme_wa_saudi_arabia_kwa_mara_ya_kumi_video
Kwa mara ya pili katika kipindi cha siku 10, rais wa Marekani ameendelea kuudhalilisha utawala wa kifalme wa Saudi Arabia akiwemo mfalme Salman bin Abdulaziz mwenyewe.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
May 11, 2019 22:05 UTC

Kwa mara ya pili katika kipindi cha siku 10, rais wa Marekani ameendelea kuudhalilisha utawala wa kifalme wa Saudi Arabia akiwemo mfalme Salman bin Abdulaziz mwenyewe.

Rais huyo wa Marekani ambaye anaonesha wazi kuwa hawaheshimu hata chembe viongozi wa Saudi Arabia, amerudia matamshi yake ya kejeli kuhusu namna Saudia isivyoweza kuishi bila ya ulinzi wa Marekani na jinsi Washington inavyoulazimisha ukoo wa Aal Saud utoe fedha nyingi kugharamia ulinzi huo. Viongozi wa Saudi Arabia wamenyamaza kimya mbele ya udhalilishaji huo wa Trump.

Siku ya Jumatano, Trump alisema wakati akizungumzia mbele ya wafuasi wake katika jimbo la Florida huko Marekani kwamba: "Utawala kama wa Saudia ni tajiri sana na hauna chochote isipokuwa fedha tu… sawasawa! Hivyo ninaamini kwamba, watawala wa Saudia wanaweza kutoa fedha nyingi za kununua ulinzi kutoka kwetu.. sawasawa!"

Mfalme wa Saudi Arabia akipeana mkono na mke wa Donald Trump alipowakaribisha Saudia

 

Rais huyo wa Marekani ambaye ni maarufu kwa kutukana pia amesema: "Wasaudia wataendelea kutoa fedha.. na wananunua vitu vingi kutoka kwetu.. wanatoa kiwango kikubwa cha fedha kununua silaha zetu kwa dola bilioni 450."

Ameendelea kuwadhalilisha viongozi wa Saudi Arabia kwa kusema mbele ya kadamnasi ya watu kwamba: "Kusema kweli kila nikiwataka watoa fedha, wananiangalia (kwa shingo upande) wakisema, hakuna mtu yeyote aliyewahi kututaka tufanye hivyo.. si kwamba wanasema maneno hayo neno kwa neno, ni wajanja, lakini mtu unaweza kupata kwa uwazi kabisa hisia kama hizo."