Uchunguzi: Wafuasi wa dini za waliowachache wananyimwa haki zao barani Ulaya
Uchunguzi umebaini kuwa, wafuasi wa dini za waliowachache wananyimwa haki zao barani Ulaya na wanaishi chini ya mashinikizo, vizuizi vikubwa na ukandamnizaji.
Gazeti la Bild la Ujerumani limechapisha matokeo ya ripoti mpya ya shirika la uchunguzi wa maoni la PEW na kuandika kuwa: Wafausi wa dini za waliowachache hawako katika hali nzuri katika nchi nyingi za kuanzia Ulaya, Marekani hadi Asia kwa kadiri kwamba, katika nchi 20 za Ulaya watu hao hawaruhusiwi hata kutumia nembo na mavazi yao ya kidini.
Shirika la uchunguzi wa maoni la PEW limeripoti kuwa, nchi kama Austria imepiga marufuku vazi Kiislamu la hijabu kwa wanafunzi mashuleni na maafisa wa serikali za Ujerumani na Uswisi wamepiga marufuku walimu kuvaa vazi hiyo. Vilevile wanafunzi wa shule za umma wamepigwa marufuku kivaa vazi la staha la hijabu au kuwa na nembo za kidini katika shule za Ufaransa.
Ripoti ya PEW ambayo imechunguza hali ya wafuasi wa dini za waliowachache katika nchi 198 duniani imesema kuwa, wafuasi wa dini za waliowachache hususan katika nchi kama Saudi Arabia wanakandamizwa kupita kiasi.
Ripoti hiyo pia imesema kuwa nchi 52 zilizofanyiwa uchunguzi zinawawekea mipaka na vizuizi vikubwa wafuasi wa dini za waliowachache katika kutekeleza ibada na desturi zao za kidini.