Jul 18, 2019 02:27 UTC
  • Sergey Lavrov: Marekani chanzo kikuu cha migogoro Mashariki ya Kati

Sergey Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema kuwa, Marekani ndio chanzo cha migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesisitiza kuwa, siasa za  serikali ya Marekani zilizo dhidi ya Jamhuri ya Kkiislamu ya Iran katika eneo la Magharibi mwa Asia zimekuwa chanzo cha migogoro katika eneo hili.

Sergey Lavrov amesema bayana kwamba, hali mbaya ya migogoro inayoshuhudiwa hii leo katika eneo hiili la Magharibi mwa Asia ina uhusiano wa moja kwa moja na siasa za serikali ya Marekani na washirika wake zilizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Rais Donald Trump wa Marekani

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia ameashiria tuhuma za Washington dhidi ya Tehran na kkusema kuwa, mwenendo huu unapelekea kujitokeza anga mbaya na hatari.

Aidha mwanadiplomasia huyo mwandamizi wa Russia ameongeza kuwa, kutokana na hali ilivyo hivi sasa ili kuwasha moto wa mzozo kinachohitajika ni kibiriti tu, ambapo watakaobeba dhima ya matokeo ya maafa haya ni serikali ya Marekani.

Lavrov ameeleza kuwa, viongozi wa Iran hawataki vita na daima wameonyesha hamu na shauku yao ya kupatikana amani na uthabiti wa eneo kupitia njia ya mazungumzo na nchi zote ambazo zina mizozo na hitilafuu zikiwemo nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.

Tags