WHO yatoa wito wa kupambana na ugonjwa wa malaria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i55556-who_yatoa_wito_wa_kupambana_na_ugonjwa_wa_malaria
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito kwa walimwengu kuwekeza zaidi katika mapambano dhidi ya malaria na kuutokomeza kikamilifu ugonjwa huo ambao kila mwaka huua watu laki nne.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Aug 23, 2019 07:10 UTC
  • WHO yatoa wito wa kupambana na ugonjwa wa malaria

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito kwa walimwengu kuwekeza zaidi katika mapambano dhidi ya malaria na kuutokomeza kikamilifu ugonjwa huo ambao kila mwaka huua watu laki nne.

Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani Ijumaa ya leo wametoa taarifa wakisema kuwa, mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria katika kipindi cha miaka miwili ya hivi karibuni yamepungua sana na kwenda mwendo wa kinyonga. 

Taarifa hiyo imesema kuwa, kila mwaka zaidi ya watu milioni 200 hupatwa na ugonjwa wa malaria kote duniani na zaidi ya laki nne miongoni mwao huaga dunia kutokana na ugonjwa huo. 

Mtoto mwenye Malaria akipata matibabu

Timu ya wataalamu wa Shirika la Afya Duniani inasema kuwa, dola bilioni 34 zinapaswa kuwekezwa katika mapambano dhidi ya malaria hadi kufikia mwaka 2030 ili kutia kasi zaidi katika mapambano dhidi ya janga hilo. 

Taarifa hiyo ya wataalamu wa WHO imetolewa baada ya Dokta Pedro L. Alonso ambaye ni Mkrugenzi wa Mpango wa Shirika la Afya Dunia wa Kupambana na Malaria kusema kuwa, mapambano dhidi ya ugonjwa huo yamekaribia kusimama kabisa tangu miaka miwili iliyopita hususan katika bara la Afrika lililoathiriwa zaidi ya ugonjwa huo.