Ujerumani yatahadharisha kuhusu kukaririwa mgogoro wa wahajiri barani Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i56505-ujerumani_yatahadharisha_kuhusu_kukaririwa_mgogoro_wa_wahajiri_barani_ulaya
Horst Seehofer Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani alitahadharisha jana katika kikao cha Mawaziri wa Nchi za Ulaya huko Brussels kuwa, kuna uwezekano wa kukaririwa mgogoro wa wahajiri barani Ulaya kama ule ulioshuhudiwa mwaka 2015.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 09, 2019 03:08 UTC
  • Ujerumani yatahadharisha kuhusu kukaririwa mgogoro wa wahajiri barani Ulaya

Horst Seehofer Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani alitahadharisha jana katika kikao cha Mawaziri wa Nchi za Ulaya huko Brussels kuwa, kuna uwezekano wa kukaririwa mgogoro wa wahajiri barani Ulaya kama ule ulioshuhudiwa mwaka 2015.

Seehofer amesisitiza kuwa kuna udharura kwa nchi za Ulaya kuchukua hatua madhubuti na zilizoratibiwa ili kuipatia ufumbuzi kadhia ya wahajiri. Amesema kuwa nchi hizo zinapaswa kusadia kukabiliana na wimbi kubwa la wahajiri kuelekea Ulaya. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Ujerumani ametoa indhari hiyo kuhusu uwezekano wa kukaririwa mgogoro wa wahajiri barani Ulaya katika hali ambayo kabla ya tahadhari hiyo; nchi za Ulaya kama Ugiriki na Cyprus zilitahadharisha kuhusu kuingia katika nchi hizo idadi kubwa ya wahajiri waktokea katika mipaka ya Uturuki. Katika miaka ya karibuni raia wengi kutoka nchi za eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika wamekuwa wakijaribu kuingia Ulaya wakiepa machafuko na hali mbaya ya kiuchumi, kijamii na kisiasa katika nchi zao iliyosababishwa na uingiliaji wa nchi za Magharibi.