Idadi ya kaya masikini nchini Ujerumani imeongezeka
-
Idadi ya kaya masikini nchini Ujerumani imeongezeka
Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa idadi ya kaya maskini nchini Ujerumani inaongezeka na kukosekana kwa usawa wa kipato kumeongezeka hadi kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, na hivyo kusababisha hali ya kutoaminiana katika nyanja za kisiasa.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari la Tasnim, likinukuu jarida moja la Uujerumani limeripoti kuwa, matokeo ya uchunguzi yanaonyesha kuwa idadi inayoongezeka ya watu wa Ujerumani wanatoka tabaka kati kuelekea chini na kuingia katika janga la umaskini.
Hii inaonyeshwa katika ripoti mpya ya usambazaji kutoka kwa Wakfu wa Hans Böckler. Utafiti huo unachanganua, miongoni mwa mambo mengine, takwimu za hivi punde zaidi za Jopo la Kiuchumi na Kijamii (SOEP) kutoka mwaka 2022.
Kulingana na ripoti hiyo, idadi ya kaya zinazoishi katika umaskini nchini Ujerumani imeongezeka hadi asilimia 17.7. Mwaka 2010, takwimu ilikuwa asilimia 14.4.
Takwimu zinaonyesha kuwa, watu wa tabaka la kati kuelekea chini wamekuwa maskini zaidi, kumaanisha kuwa wamepata mapato kidogo.
Moja ya matokeo hayo ni kwamba, ukosefu wa usawa wa mapato umeongezeka nchini Ujerumani.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs) yanaonekana kuongezeka kwa kiwango cha kuogofya nchini Ujerumani.
Idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa zinaa wa kaswende imefikia rekodi mpya ya kutisha nchini Ujerumani, na kufikia kesi 9,519 mnamo 2024 ikilinganishwa na 1,697 tu mwanzoni mwa karne hii, kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni kutoka Taasisi ya Robert Koch (RKI).