Waziri Mkuu wa Malaysia aonya kuongezeka uingiliaji wa kigeni nchini Sudan
-
Majenerali hasimu wa Sudan ambao wameitumbukiza nchi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe
Waziri Mkuu wa Malaysia ameonya kuhusiana na kuongezeka kwa uingiliaji wa kigeni nchini Sudan.
Anwar Ibrahim ameonya dhidi ya kuongezeka kwa uingiliaji wa kigeni nchini Sudan, akisema: "uingiliaji huu si tu utasababisha kuongezeka kwa mzozo lakini pia utazuia juhudi zozote za dhati za utatuzi wa kisiasa."
Ameongeza kuwa,"Kuna dalili za wazi kwamba pande kuutoka nje zinahusika katika kuimarisha mgogoro nchini Sudan. Kuendelea na mbinu hii kutaongeza muda wa vita na kuongeza mateso na ugumu wa maisha ya raia. Tunatoa wito kwa pande zinazohusika kusitisha mapigano mara moja na kujihusisha na mazungumzo ya kisiasa ya kujumuisha watu wote," aliiambia Al Jazeera.
Tangu katikati ya Aprili 2023, Sudan imekuwa katika mzozo wa kijeshi kati ya jeshi la taifa na waasi wa RSF ambao umesababisha vifo vya makumi ya maelfu na watu na kuwalazimisha wengine milioni 13 kuhama makazi yao.
Baada ya kudhibiti mji wa El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vimetuma sehemu kubwa ya wapiganaji wake katika jaribio la kudhibiti miji mikubwa katika eneo la Kordofan.
Chanzo cha kijeshi katika jeshi la Sudan kimesema kwamba vikosi vya jeshi vinapambana na waasi wa RSF katika miji kadhaa katika jimbo la Kordofan Kaskazini.