Askari watano magaidi wa Marekani wajeruhiwa kusini mwa Afghanistan
Shambulio la guruneti la wapiganaji wa kundi la Telaban dhidi ya kambi ya askari magaidi wa Marekani kusini mwa Afghanistan, limepelekea magaidi watano miongoni mwa askari hao kujeruhiwa.
Viongozi wa jimbo la Helmand, kusini mwa nchi hiyo wamenukuliwa wakisema kuwa, wapiganaji wa kundi la Taleban wameshambulia kambi ya askari hao magaidi wa Marekani katika mji wa Lashkar Gah, makao makuu ya jimbo hilo. Katika shambulizi hilo askari watano magaidi wa Kimarekani wamejeruhiwa ambapo baadhi wana hali mbaya. Kabla ya hapo pia Zabiullah Mujahid, Msemaji wa kundi la Taleban alitangaza kuwa, askari wanane wa Marekani waliangamizwa na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu lililokuwa limetegwa barabarani.

Kwa mujibu wa msemaji huyo wa Taleban, askari hao magaidi wa Marekani walikuwa wakitembea katika mji wa Bagram, makao makuu ya jimbo la Parwan nchini Afghanistan. Wakati huo huo, askari wa serikali ya nchi hiyo wamefanikiwa kuukomboa mji wa Darqad wa jimbo la Takhar, kaskazini mwa Afghanistan kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Taleban. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imesema kuwa, maafisa usalama kwa kushirikiana na jeshi la nchi hiyo wamefanikiwa kuukomboa mji huo asubuhi ya leo kupitia operesheni ya kali ya kijeshi, iliyoanza wiki mbilizi zilizopita, huku wapiganaji 50 wa kundi la Taleban wakiuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.