Ndege ya Iran iliyobeba msaada wa COVID-19 yawasili Venezuela
(last modified Tue, 09 Jun 2020 08:04:43 GMT )
Jun 09, 2020 08:04 UTC
  • Ndege ya Iran iliyobeba msaada wa  COVID-19 yawasili Venezuela

Serikali ya Venezuela imesema ndege ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliyobeba msaada wa dharura kwa ajili ya waathirika wa ugonjwa wa COVID-19 iliwasili nchini humo jana Jumatatu.

Iran imetuma msaada huo wa kibinadamu nchini Venezuela baada ya wataalamu wa afya kuonya kuwa, nchi hiyo ya Amerika ya Latini ipo katika hatari kubwa ya kuathiriwa vibaya na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 (corona) kutokana na kusambaratika huduma za afya, maji na umeme kufuatia vikwazo haramu vya Marekani.

Siku ya Jumapili, Rais Nicolas Maduro wa Venezuela alisema misaada ya dharura na ya kibinadamu iliyotumwa nchini humo na Iran, Russia, China na Cuba inaonesha kuwa nchi hizo ndio marafiki wa kweli wa Venezuela.

Wananchi wa Venezuela wakionyesha furaha baada ya kuwasili meli za mafuta ya Iran

Hivi karibuni Iran ilituma meli tano za bidhaa za petroli nchini Venezeula licha ya vitisho pamoja na kuwepo vikwazo haramu vya Marekani, na hatua hii imetajwa na weledi wa mambo kuwa mafanikio makubwa kwa Iran.

Kufuatia hatua hiyo ya Iran, serikali ya Caracas inayokabiliwa na vikwazo vikali sasa imeweza kuanzisha mfumo mpya wa kusambaza petroli na dizeli nchini humo.

Tags