Kansela wa Ujerumani asisitiza kuhusu nafasi ya jiostratejiki ya Russia kimataifa
Kansela wa Ujerumani amesema kuwa Russia ni nchi iliyo na nafasi ya jio-stratejiki na ametaka mazungumzo yafanyike kati ya Berlin na Moscow.
Bi Angela Merkel ameeleza kuwa Russia ikiwa nchi yenye nafasi ya jiostratejiki ina mchango muhimu katika kadhia mbalimbali za kimataifa kama zile za Syria na Libya na kuongeza kuwa: kuna udharura wa kushirikiana zaidi Berlin na Moscow katika uwanja huo kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
Kansela wa Ujerumani amesema kuwa, Russia ni nchi kubwa yenye historia kongwe na utamaduni tajiri na kusistiza kuwa kuimarisha uhusiano na Moscow ni katika vipaumbele vya ajenda za siasa zake za nje.
Kukiri Kansela wa Ujerumani ambayo inahesabiwa kuwa nchi muhimu zaidi katika Umoja wa Ulaya na yenye nafasi nyeti ndani ya umoja huo na katika Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato) kuhusu nafasi muhimu ya Russia katika kadhia za kimataifa kunaashiria kubadilika misimamo ya kambi ya Magharibi mkabala na taswira na nafasi iliyonayo sasa Russia duniani.