Biden: Trump 'ameifedhehesha' Marekani mbele ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i63410-biden_trump_'ameifedhehesha'_marekani_mbele_ya_iran
Joe Biden, mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrats amesema, siasa za Donald Trump kuhusu Iran zimefeli na zimeifedhehesha Marekani kwa kuifanya itengwe kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 13, 2020 22:39 UTC
  • Biden: Trump 'ameifedhehesha' Marekani mbele ya Iran

Joe Biden, mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrats amesema, siasa za Donald Trump kuhusu Iran zimefeli na zimeifedhehesha Marekani kwa kuifanya itengwe kimataifa.

Biden amenukuliwa na televisheni ya CNN akisema hayo jana na kuongeza kuwa, siasa za serikali ya Donald Trump zimefeli mbele ya Iran na kwamba rais huyo alifanya kosa na alitenda kinyume na maslahi ya Marekani kwa hatua yake ya kujitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA.

Amesema, kwa hatua yake hiyo, Trump ameifanya Marekani itengwe kimataifa kiasi kwamba katika majaribio mawili ya Washington dhidi ya Iran katika suala la kutaka kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Tehran, Marekani imeshindwa hata kupata uungaji mkono wa waitifaki wake wa karibu kabisa kama vile nchi za Ulaya.

Donald Trump, rais wa Marekani aliyevurunda kila upande

 

Biden amegusia pia mashambulio ya makombora yaliyofanywa na Iran dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Iraq na kupelekea zaidi ya wanajeshi 100 wa Marekani kupata matatizo ya ubongo akisema, baada ya mashambulio hayo, Trump alitaka kuonesha kuwa hayakuwa mashambulizi makubwa na alidharau madhara waliyopata wanajeshi wa Marekani kwa kudai kwamba wanajeshi hao walikuwa wanaumwa na kichwa tu.

Amesema, kama atachaguliwa kuwa Rais wa Marekani atabadilisha siasa hizo za Trump na atarejesha muungano uliopatikana kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA wa kile alichodai ni kuizuia Iran kuwa na silaha za nyuklia. Pia amesema serikali yake itatumia njia za kidiplomasia kuamiliana na kadhia ya Iran.