Grossi apongeza ushirikiano wa Iran na wakala wa IAEA
https://parstoday.ir/sw/news/world-i63426-grossi_apongeza_ushirikiano_wa_iran_na_wakala_wa_iaea
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) amepongeza ushirikiano mzuri wa Iran na taasisi hiyo ya kimataifa baada ya kufanyika kikao cha Bodi ya Magavana ya wakala huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 14, 2020 22:06 UTC
  • Grossi apongeza ushirikiano wa Iran na wakala wa IAEA

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) amepongeza ushirikiano mzuri wa Iran na taasisi hiyo ya kimataifa baada ya kufanyika kikao cha Bodi ya Magavana ya wakala huo.

Rafael Grossi jana Jumatatu alitoa jibu chanya katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kikao cha Bodi ya Magavana ya wakala wa IAEA pale alipoulizwa na mwandishi habari kwamba, je Iran imeetoa mashirikiano yanayohitajika kwa wakala huo wa kimataifa au la. 

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki ameitaja hatua ya Iran ya  kuuruhusu wakala wa IAEA kuyakagua maeneo mawili hapa nchini kuwa ni tukio chanya. 

Kuhusu muda wa kuchunguza sampuli zilizotolewa katika eneo la kwanza ambalo limekaguliwa na wakala wa IAEA hapa Iran, Grossi amesema: Hawezi kukadiria muda maalumu katika uwanja huo laini suala hilo litachukua muda wa chini ya miezi miwili hadi mitatu. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Wakala wa IAEA tarehe 26 mwezi Agosti mwaka huu zilitoa taarifa ya pamoja mwishoni wa safari ya siku mbili ya Rafael Grossi hapa Tehran na kufuatia mazungumzo kati yake na viongozi wa Iran.  

Ali Akbar Salehi, Mkuu wa Taasisi ya Nyuklia ya Iran katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA mjini Tehran, Rafael Grossi

Taarifa hiyo ya pamoja ilieleza kuwa: Iran, kwa hiyari yake, imeruhusu  kukaguliwa maeneo mawili yaliyoainishwa na wakala huo ili kufanikikisha shughuli za uhakiki na kuyapatia ufumbuzi masuala hayo.  

Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati Nyuklia jana Jumatatu ilifanya kikao chake cha mwezi Septemba ambapo ajenda mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo kadhia ya Iran, mapatano ya JCPOA na suala la usalama katika eneo la Asia Magharibi.