Utafiti wa Gallup: nchi za ulimwengu zinashindwa kuvumilia kuwapokea wakimbizi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i63595-utafiti_wa_gallup_nchi_za_ulimwengu_zinashindwa_kuvumilia_kuwapokea_wakimbizi
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Gallup unaeleza kuwa nchi mbalimbali zinashindwa kuvumilia kuwapokea wakimbizi.
(last modified 2025-11-19T02:13:06+00:00 )
Sep 23, 2020 12:18 UTC
  • Utafiti wa Gallup: nchi za ulimwengu zinashindwa kuvumilia kuwapokea wakimbizi

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Gallup unaeleza kuwa nchi mbalimbali zinashindwa kuvumilia kuwapokea wakimbizi.

Utafiti huo umebainishwa huku Ulaya ikijiandaa kuzindua mpango wake mpya kufuatia kutokea moto kwenye kambi moja inayohifadhi idadi kubwa ya wahajiri nchini Ugiriki na kusababisha maelfu ya wakimbizi hao kukosa makazi. 

Utafiti huo wa Gallup unaeleza kuwa, nchi saba za Ulaya zikiongozwa na Macedonia Kaskazini, Hungary, Serbia na Croatia ndizo zinazoongoza katika orodha ya dunia ya nchi zinazopokea idadi ndogo wakimbizi. 

Nchi ya Canada imetajwa kuwa nchi yenye kupokea sana wakimbizi ikifuatiwa na Iceland na New Zealand. Hiyo ni kwa mujibu wa mahojiano zaidi ya 140,000 yaliyofanywa katika nchi na maeneo 145 duniani.  Matokeo ya utafiti huo yamepatikana baada ya watu mbalimbali kutakiwa kutoa maoni yao kuhusu kuwapokea wahajiri nchini mwao na watu hao kuwa majirani na kuoa katika familia zao. 

Canada ni nchi inayopokea sana wakimbizi duniani  

Nchi za Ulaya zimekuwa zikikabiliwa na wimbi kubwa la wakimbizi ambao wengi wao wanatoka katika nchi zinazopakana na bahari ya Medireania wanaofika Ulaya baada ya safari ngumu za boti dhaifu. 
Kamati ya Umoja wa Ulaya leo Jumatano ilipanga kuzindua mpango wake huo ambao utazilamisha kisheria nchi zote wanachama kila mmoja kupokea mgao wake wa wakimbizi. Poland na Hungary zimeupinga mpango huo.